Jumatatu, 9 Septemba 2013

 

SERA YA MANUFAA KWA UMMA 

Ilikuwa tarehe 14/08/2013 nilipotembelea sehemu ambayo nilisoma nikiwa kidato cha sita (Mwakaleli sekondari). Sehemu yenyewe ni kandete kwenye kijiji cha Lugombo na kukutana na uzuri na ubaya wa mambo kadhaa. Nilikutana na kibao nilicho pendezwa nacho kuhusu utunzaji wa mazingira ya kwetu.

 

Lakini japo kuwepo kwa sera hiyo ninayoiita ya manufaa bado inaonesha utekelezaji wa sera huo ni mbovu kwani mito imejaa majani ikionesha kuwepo kilimo karibu na vyanzo vya maji. Hapo awali maeneo hayo yalifurika kwa maji mengi hasa kwa kipindi hicho.






 JAMII INATAKIWA KUJUA KUWA INAWAJIBU WA KUTUNZA NA KULINDA AMALI ZA JAMII HUSIKA KWA KIZAZI KIJACHO.

 KUNA BAADHI YA MITI YA ASILI TUSIPO ITUNZA ITAPOTEA KWA JUMLA

TUTUNZE ARDHI YETU KWA MANUFAA YA WOTE