Jumamosi, 24 Januari 2015

Tehama shuleni; Dhamira njema iliyokosa mikakati wezeshi

Kwa ufupi. Pamoja na dhamira njema ya Serikali kutaka Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutumika, mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji, imeshindwa kuandaa mazingira ya kuwezesha teknolojia hiyo kufanya kazi katika shule za msingi na sekondari hasa zile za umma.

Soma kisa hiki; Mgeni anakuja nchini na kutaka pamoja na mambo mengine kuwafundisha kompyuta watu wa jamii ya wafugaji ambao asili yao ni maisha ya kuhamahama porini.
Mkutano unaitishwa na mkataba wa makubaliano unawekwa kati yake na watendaji wa Serikali ili atoe elimu hiyo vijijini. Baada ya mkutano sote tunashangilia.
Hadithi hii inashabihiana na yanayotokea sasa katika sekta ya elimu nchini. Ilivyo ni kuwa baadhi ya mipango ya kielimu haina tija kwa kuwa haitekelezeki, japo dhamira yake ni nzuri.
Kama haitoshi mipango hiyo siyo kipaumbele muhimu kwa jamii licha ya ukweli kuwa imekuwa ikianzishwa kwa mbwembwe na ahadi lukuki.
Tehama shuleni
Kilele cha maono duni ya wale waliopewa jukumu la kusimamia elimu yetu, linajionyesha katika mipango iliyopo ya kutaka zana za kisasa za Tehama zitumike katika kufundishia na kujifunzia shuleni.
Mfano mzuri ni mpango wa hivi karibuni ambapo , Serikali kwa kushirikiana na kampuni za Vodacom na Samsung wameanzisha mpango wa kuziunganisha shule za sekondari nchini na mkongo wa mawasiliano wa taifa.
Hatua hiyo itatoa fursa kwa shule kutumia kompyuta zilizounganishwa na intaneti katika kufundishia na kujifunzia.
Hata hivyo, pamoja na dhamira hii njema, swali la msingi ni je, shule hizo zina miundombinu tayari kwa kuunganishwa na mkongo wa mawasiliano?
Kinachoshangaza ni kuwa mipango yote hii inabuniwa ilhali hakuna mikakati ya kuweka mazingira wezeshi shuleni, kama vile uwepo wa nishati ya umeme ambayo ni muhimu katika matumizi ya Tehama.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, hadi mwaka 2012 shule mbili za msingi na tano za sekondari (wasioona) ndizo zilizokuwa zimenufaika na mradi huo wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kati ya maelfu ya shule zilizopo nchini.
Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa shule za msingi zilizonufaika ni Buigiri (Dodoma) na Kizega (Singida). Shule za sekondari zilizonufaika mpango huo ni Ilula (Iringa), Mpwapwa (Dodoma), Ilowola (Njombe), Tumaini na Lulumba (Singida).



A bad practice To a women around the world.

we need to be awaken from the sleepy of lie, by thinking we save our relationships with our partners while we endanger our Health. 

Women around the world are carrying out a practice which not only leaves them in pain but at increased risk of HIV and other sexual transition Diseases (STD's). 

Women around the world are carrying out a practice of 'drying out' their vaginas to make sex more pleasurable for men - a practice which not only leaves them in pain but at increased risk of HIV.

'Dry sex' involves women reducing moisture in their vaginas in order to make intercourse more pleasurable for men, according to the Daily Mail report.

“Dry sex is known to be carried out in South and Central Africa, and Indonesia,” the report says. “It is borne out of a cultural belief that men find sex more pleasurable if a woman's vagina is dry, and that men will reject women whose vaginas have been ‘stretched out’ by sex.

“To achieve dryness, women insert, chalk, sand, pulverized rock, herbs, paper or sponges before sex, according to journalist Ms Wendy Syfret, who has reported on the practice in South Africa.

“They also douse their vaginas in detergents, antiseptics, alcohol and bleach. This can lead to cuts, sores and inflammation in the vagina, and increases the chance of a condom breaking.”

   

Profesa Sospeter Muhongo atangaza kijiuzuru kufuatia sakata la Tegeta-Escrow

 
HATIMAYE Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo leo ikiwa ni karibu mwezi mmoja tangu kuwepo kwa shinikizo la kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
Prof Muhongo ni miongoni mwa waliotajwa katika kashfa hiyo, lakini hakuchukuliwa hatua zozote na Rais Jakaya Kikwete wakati akilihutubia taifa, huku aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka akiondolewa kwenye nafasi yake kutokana na sakata hilo.
Maamuzi ya kuachia ngazi kwa Prof Muhongo yametolewa mbele ya wanahabari aliokutana nao asubuhi jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kueleza mafanikio yake ndani na nje ya nchi kupitia wizara hiyo na kujitaja kama mtu msafi ambaye ana doa lolote, waziri huyo alitangaza kuachia ngazi kwa madai ya kutafakari kwa kina, ingawa kabla ya hapo alishawahi kunukuliwa kwamba asingejiuzulu ng'o.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wakubwa wake, ikizangatiwa heshima aliyonayo kama Profesa.
Kujiuzulu kwake kumekuwa wakati Katibu wake, Eliakim Maswi kutimuliwa kazini na Katibu Mkuu Kiongozi kutokana na sakata hilo, huku watendaji kadhaa umma wakiburuzwa mahakamani wakikabiliwa na kesi zinazohusiana na sakata hilo la Tegeta Escrow.



Jumanne, 20 Januari 2015


 

Mercedes-Benz reveals Future Truck 2025, the Optimus Prime of self-driving semis


Motoramic

Mercedes-Benz Future Truck 2025
.
View gallery

Mercedes-Benz Future Truck 2025
U.S. trucking firms have long complained that they have more jobs than drivers — about 30,000 more, according to the most recent figures from the American Trucking Association. And who can blame someone for choosing another profession, what with the weeks on the road away from family and the stress of just-in-time delivery schedules for the chance to earn an average of $50,000 a year.
Today, Mercedes-Benz revealed the full details of how it sees the trucks of the future making the drivers of today more of a profession than a trade — with an Optimus Prime-like rig that can drive itself while the "transport manager" types away in his luxury studio.
Mercedes had previously shown a camouflaged version of the Future Truck 2025 that highlighted its autonomous driving abilities with a full load up to 50 mph, an expanded version of what the company already offers to buyers of the new S-Class coupes and sedans. Wolfgang Bernhard, head of Mercedes' truck division, has said autonomous driving would be the future of trucking, but one that was still a decade away given higher technological and legal hurdles.

What Mercedes had not shown before was just how radical it imagined the look of the Future Truck to be. Start with the front, where there are no headlamps — the Future Truck uses fields of LEDs embedded across its fascia to light its path, which glow from underneath its skin. They don't just beam one color, but change colors from white to a shade of purple and pulse slowly to indicate a truck that's driving itself.
The radical rethink extends to the cabin, where Mercedes has tried to answer the question of what a truck driver will do if he or she doesn't have to drive for several hours. In place of the bank of controls in a modern semi, Mercedes has reduced most of the necessary info into a few screens, turning the cabin into a expanse of wood and leather like a high-end New York hotel room. The driver's seat swivels 45 degrees to the right, so that a driver can stretch out when controlling the truck through its iPad-like touchscreen. And there's a digital picture frame in back for remembering the family while on the road.
In that one flourish, Mercedes may be trying to assuage worries that Future Truck and similar projects will eliminate jobs rather than alter them, making truck driving more white collar, or like the ultimate telecommuter. "The profession of truck driver will become more attractive – autonomous driving is therefore also a compelling answer to the shortage of drivers," the company said today. "With autonomous driving, the truck and its driver become a team more than ever before, an intelligent, highly capable and cost-effective combination of man and machine." We may not know before 2025 whether Future Trucks will serve as a real-life Optimus Prime — or become an economic Decepticon for drivers.

Jumamosi, 6 Septemba 2014

NGUO ZA MITUMBA NI HATARI SANA HEBU ONA HAPO CHINI

Hao unaowaona kama weusi weusi kwenye ziwa hapo ni funza ambao wameform matobo matobo ambapo wanatoka nje sasa baada ya kukomaa ki ukweli tunatakiwa tuwe makini sana na nguo hizi za mitumba tunatakiwa tuzifue kwa maji ya moto ili kuua vimelea na madawa yaliyopuliziwa vinginevyo tutaumia sana na hii pia ni fundisho kwa wale wenye kuvaa nguo za ndani za mitumba pia bila kuzifua wadada na wakaka tuweni makini kwenye mavazi yetu ukiona ujumbe huu mtaarifu na mwenzio auone SHARE kwa manufaa ya wengine. Asanten

Alhamisi, 27 Februari 2014

SISI NA KATIBA MPYA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto), akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kabla ya kuanza kikao cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma jana. Picha:Selemani Mpochi.

 

Mwenyekiti Bunge la Katiba nguvu kwa Migiro,Chikawe


  Yadaiwa ni baada ya mambo kumemwendea vibaya Chenge
Waziri wa Katiba na Sheria,Dk. Asha-Rose Migiro.
Kampeni  za makundi ya vigogo wanaopigana vikumbo kugombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba zimechukua sura mpya, baada ya kundi lililokuwa likimuunga mkono Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge kudaiwa kubadili ghafla mwelekeo wa kampeni zake.

 Habari za kuaminika zilizopatikana mjini hapa jana zilieleza kuwa kundi hilo lililokuwa likimtaka Chenge, sasa linataka nafasi hiyo iwaniwe na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro au Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

 Hatua hiyo inadaiwa kuchukuliwa na kundi hilo baada ya kubaini kuongezeka kila uchao kwa nguvu za Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye tayari ameshatangaza kuwania nafasi hiyo, huku zile walizozitarajia kutoka kwa Chenge zikizidi kushuka.

 Habari hizo zinaeleza kuwa uthibitisho wa hilo, ni ujasiri ulioonyeshwa na Sitta aliyeamua kutangaza hadharani azma yake ya kuwania nafasi hiyo, huku Chenge akishindwa kuthibitisha kuwa atagombea ama la.

Uchaguzi wa mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba unatarajiwa kufanyika Jumapili wiki hii baada ya Bunge hilo kupitisha azimio la kuipitisha rasimu ya kanuni za Bunge Maalumu kesho.

Awali, Chenge aliiambia NIPASHE kuwa hayuko tayari kutangaza kama atagombea nafasi hiyo au la kwa kuwa kanuni za Bunge hilo bado hazijatungwa.

Kauli kama hiyo iliwahi pia kutolewa na Waziri Sitta katika siku hiyo hiyo, ambayo Chenge aliashiria kusubiri kanuni.

Hata hivyo, siku chache baadaye, hata kabla ya rasimu ya kanuni hizo haijapitishwa na Bunge, Waziri Sitta alitangaza azma yake ya kugombea nafasi hiyo kwa maelezo kwamba, anataka kutimiza ndoto ya Rais Jakaya Kikwete ya kupata katiba bora.

Jumatatu wiki hii, Chenge alipoulizwa na NIPASHE kuhusiana kinyang'anyiro hicho, alikataa kuzungumza na badala yake akamtaka mwandishi aendelee na shughuli zake.

Waziri Chikawe alipotafutwa na NIPASHE jana kuzungumza kama ana nia ya kugombea nafasi hiyo au la, alimtaka mwandishi kuvuta subira kwa kuwa wakati huo hakuwa na nafasi ya kuzungumza.

Dk. Migiro ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) hakupatikana
kuzungumzia suala hilo.

Jitihada za kuwatafuta viongozi hao wanaotajwa kuwania nafasi hiyo zinaendelea.
CHANZO: NIPASHE

Ijumaa, 18 Oktoba 2013

JK, Mbowe, Lipumba,Mbatia wakubaliana

16th October 2013
Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Ikulu jijini Dar es Salaam jana baada ya mazungumzo na viongozi vyama vya upinzani. Nyuma kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba.

Rais Jakaya Kikwete jana alikutana na viongozi wa vyama sita vya siasa vyenye uwakilishi bungeni, Ikulu, jijini Dar es Salaam na kukubaliana mambo makuu mawili.

La kwanza, vyama vyote vya siasa vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2013, kuyawasilisha haraka serikalini ili kutafuta namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.

La pili, vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano wa jinsi kwa pamoja vitakavyosukuma mbele mchakato mabadiliko ya katiba ya nchi kwa maslahi mapana ya nchi na mustakabali wa taifa.

Katika makubaliano hayo, Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, mkutano kati ya Rais Kikwete na viongozi ulimalizika jana jioni na pande mbili hizo kukubaliana mambo hayo.

Viongozi wa ambao Rais Kikwete alikutana nao jana kwa mazungumzo hayo wanatoka vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP.

Viongozi hao walianza kuwasili kwa nyakati tofauti, kuanzia saa 6:00 mchana jana na kupokelewa na maofisa usalama wanaotoa huduma mapokezi, Ikulu, kabla ya kuelekezwa kwenye chumba maalumu kilichoandaliwa kwa ajili ya mazungumzo kati yao na Rais Kikwete.

Walioanza kuwasili Ikulu katika muda huo, ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, James Mbatia, akiongozana na Martin Mng’ong’o kutoka chama hicho.

Baada ya Mbatia kuwasili Ikulu muda mfupi, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alifika ambaye ndiye msemaji wa viongozi hao.

Profesa Lipumba aliongozana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Julius Mtatiro na Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Mohammed Habib Mnyaa.

 Dakika chache baadaye, aliwasili Mwenyekiti wa Chadema, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

Mbowe aliongozana na Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa Chadema, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika.

Viongozi hao walifuatiwa na wenzao kutoka CCM, UDP na TLP kuwasili Ikulu muda mfupi baadaye.

Hao ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula; Isaack Cheyo, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa UDP, ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.

Wengine ni Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema.

Ujumbe wa serikali pia iliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, baadaye jana jioni, Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa viongozi hao walikutana na Rais Kikwete, Ikulu katika mazingira ya maelewano na mwafaka.

Katika mazungumzo hayo, vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi viliwasilisha waraka wa ushirikiano wa vyama vya upinzani kwa Rais Kikwete.

Waraka huo unamshauri Rais Kikwete kutumia mamlaka yake ya Kikatiba kukataa kuukubali muswada huo, ambao vyama hivyo viliulalamikia kuwa una kasoro.

Muswada huo uliopitishwa na Bunge Septemba 6, mwaka huu, unasubiri kusainiwa na Rais ili uanze kutumika kama sheria rasmi.

“Ushauri wetu unatokana na imani yetu kwamba endapo muswada huu utapata ridhaa yako na kuanza kutumika kama sheria utakuwa na madhara makubwa kwa mchakato mzima wa utungaji wa Katiba Mpya na kwa amani na utulivu wa nchi,” inaeleza sehemu ya waraka huo uliosainiwa na Mbowe, Profesa Lipumba na Mbatia.

USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA WANANCHI

Waraka huo unataja sababu mbalimbali za tishio hilo kuwa ni pamoja na ushirikishwaji hafifu wa wananchi, hasa wadau wa kitaasisi au binafsi kutoka Zanzibar katika kuuchambua na kuutolea maoni muswada huo.

USHIRIKISHWAJI HAFIFU WA SMZ
Sababu nyingine ni ushirikishwaji hafifu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari, aliwahi kukaririwa akisema hadharani kwamba ushirikishwaji wa SMZ ulihusu vifungu vinne tu vya muswada huo.

Lakini akasema vifungu vingine vyote vya muswada vilivyopitishwa na Bunge havikupelekwa Zanzibar na kwa hiyo, SMZ haikushirikishwa kwenye kuvitolea maoni na msimamo.

BUNGE MAALUMU LA KATIBA
Waraka huo unadai kuwa muswada huo umefanya mabadiliko makubwa kuhusu utaratibu wa kuunda Bunge Maalumu la Katiba, ikiwamo Rais kuwa na mamlaka kisheria ya kuteua wajumbe 166 wa Bunge hilo wasiokuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Pili, siyo lazima tena kwamba wajumbe hao 166 watokane na makundi ya kijamii.

“Mabadiliko haya hayakuwapo kwenye Muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni mwezi Mei mwaka huu, na wala hayakutolewa maoni na wadau walioalikwa mbele ya Kamati. Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikujulishwa juu ya marekebisho haya na wala haikuyatolewa maoni na msimamo wake,” unaeleza waraka huo.

IDADI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU
Waraka huo unasema Bunge hilo litakuwa na wajumbe 604, yaani wabunge 357, wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 81 na wajumbe wengine 166.

“Hali hii isiporekebishwa itakuwa na maana kwamba Katiba Mpya itatokana na matakwa ya vyama vya siasa ambavyo idadi ya jumla ya wanachama wao haifiki milioni kumi kati ya Watanzania zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,” unaeleza waraka huo.

Mengine yanahushu uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalumu la Katiba, utaratibu wa kupitisha Katiba Mpya kwenye Bunge Maalumu, ukomo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuingizwa kwenye muswada mambo ambayo hayakujadiliwa wala kupitishwa na Bunge.

“Kwa ajili hiyo, tunakuomba utumie mamlaka yako kama Rais na Mkuu wa Nchi yetu chini ya ibara ya 97(2) ya Katiba, ukatae kuukubali muswada huu na badala yake uelekeze urudishwe Bungeni kwa sababu ambazo tumezieleza katika maelezo yetu haya,” unaeleza waraka huo.

CHANZO: NIPASHE